John Pombe Magufuli ametuma salamu za
rambirambi kwa familia za watu 30 waliopoteza
maisha katika ajali ya barabarani iliyosababishwa
na mabasi mawili ya kampuni moja ya City Boy
kugongana uso kwa uso katika kijiji cha Maweni,
kilichopo katika tarafa ya Kintinku, Wilaya ya
Manyoni Mkoani Singida.
Ajali hiyo imetokea leo tarehe 04 Julai, 2016
majira ya saa tisa alasiri wakati basi moja la
kampuni ya City Boy lenye namba T531DCE
lililokuwa likisafiri kutoka Jijini Dar es salaam
kwenda Kahama Mkoani Shinyanga lilipokuwa
likipishana na basi jingine la kampuni hiyo hiyo ya
City Boy lenye namba T247DCD lililokuwa likisafiri
kutoka Kahama Mkoani Shinyanga kwenda Jijini
Dar es salaam.
Rais Magufuli ametuma salamu zake kwa familia
zilizopatwa na msiba huo kupitia kwa Mkuu wa
Mkoa wa Singida Mhandisi Methew Mtigumwe na
kuelezea masikitizo yake juu ya kutokea kwa ajali
hiyo mbaya, iliyosababisha watu wengi kufariki
dunia.
"Nimepokea kwa mshituko mkubwa taarifa za ajali
hii ambayo imesababisha vifo vya idadi kubwa ya
watanzania, kwa hakika nimesikitishwa sana sana
na napenda kuungana na familia, ndugu, jamaa na
marafiki wa marehemu katika kipindi hiki kigumu
cha majonzi.
"Namuomba Mwenyezi Mungu awape uvumilivu na
ustahimilivu wanafamilia wote waliopoteza jamaa
zao, na sote tuwaombee marehemu wote
wapumzishwe mahali pema peponi, amina."
Ameeleza Rais Magufuli.
Aidha, Dkt. Magufuli amewaombea majeruhi wote
wa ajali hiyo, ambao wanapatiwa matibabu
hospitali wapate nafuu na kisha kupona haraka ili
warejee majumbani kwao kuungana na familia zao
katika shughuli za kila siku.
Chapisha Maoni