0
Polisi mkoani Mwanza wamekamata silaha moja
aina short gun huku mtuhumiwa wa ujambazi na
mauaji ya msikitini akitoroka akiwa chini ya ulinzi
wa askari.
Taarifa ya jeshi la Polisi mkoani mwanza inaeleza
kuwa mnamo tarehe 03.07.2016 majira ya 08:00
usiku katika maeneo ya mlima wa Kiloleli Nyasaka
wilaya ya Ilemela mkoa wa Mwanza, mtuhumiwa
wa ujambazi katika maduka ya kutuma pesa kwa
njia ya simu, pamoja na mauaji ya msikitini
aliyejulikana kwa jina Hamisi Juma miaka [38]
makazi wa Nyegezi aliyekuwa anashikiliwa na
askari, alitoroka ulinzi wa askari, wakati
akiwapeleka askari wa upelelezi kuwaonyesha eneo
lingine wanapojificha majambazi wenzake.
Aidha baada ya askari kufika kwenye eneo la tukio
ghafla majambazi waliokuwa wamejificha katika
mlima tajwa hapo juu walianza kurusha risasi kwa
askari ndipo askari walipo taharuki na kuanza
kujibu mashambulizi ya risasi kwa majambazi hao.
Pindi majibizano ya risasi yakiendelea kati ya
watuhumiwa wa ujambazi ambao walikuwa
wamejificha kwenye mlima, hali hiyo ilipelekea
mtuhumiwa bwana Hamisi Juma aliyekuwa chini
ya ulinzi wa askari polisi kupata mwanya na
kuwatoroka askari na kutokomea kusiko julikana.
Aidha a katika mapigano hayo askari walifanikiwa
kukamata bunduki aina ya short gun ilyokatwa
mtutu na kitako iliyokuwa na risasi moja chemba
iliyotupwa na majambazi hao.
Hata hivyo taarifa hiyo imesema kuwa juhudi za
kutafuta mtuhumiwa huyo zinaendelea na
kuhakikisha anatiwa nguvuni na jeshi la polisi.
Katika tukio lingine la tarehe tajwa hapo juu majira
ya saa 08:45 usiku katika eneo la Kiloleli kata ya
Nyasaka wilaya ya Ilemela mkoa wa mwanza,
mtuhumiwa wa ujambazi katika maduka ya kutuma
na kupokea pesa kwa njia ya simu, pamoja na
mauaji ya msikiti wa Rahmani uliopo kata ya
Mkolani aitwaye Mohamedi Bishof miaka [31]
shombe wa kiarabu mkazi wa Nyasaka aliruka
kutoka ndani ya gari la polisi kwa nia ya kutaka
kutoroka, lakini hata hivyo alianguka barabarani na
kuumia kichwani na sehemu mbalimbali za mwili
wake.
Aidha mtuhumiwa huyo wa ujambazi alifariki dunia
njiani wakati akipelekwa hospitali kupatiwa
matibabu.
Taarifa ya jeshi hilo inasema kuwa wakati wa uhai
wake marehemu alikiri kuwa ni kweli alihusika
katika matukio ya mauaji na unyang’anyi wa
kutumia silaha katika vibanda vya m-pesa, tigo
pesa na airtel money.
Pindi marehemu anakamatwa alikutwa akiwa na
electronic devices aliyokuwa akitumia kufanyia
matukio ya uhalifu jijini Mwanza na nje ya Mwanza
pamoja na kompyuta mpakato moja aina ya dell
ambayo walikuwa wamepora katika tukio moja la
unyang’anyi wa kutumia silaha katika tukio la
tarehe 05.05.2016 katika eneo la Kishiri Center
ambapo mwenye duka aliyejulikana kwa jina la
Phares Gabriel alijeruhiwa na risasi kwenye mguu
wa kulia na mkono wa kulia na kupora fedha
ambazo hazijafahamika zilikuwa ni kiasi gani.
Majeruhi aliyepigwa risasi katika tukio hilo
alipelekwa hospitali ya rufaa ya Bugando kupatiwa
matibabu lakini baadaye alifariki dunia kutokana na
majeraha ya risasi alizopigwa.
Mwili wa marehemu mtuhumiwa upo hospitali ya
rufaa ya Bugando kwa uchunguzi na utambuzi.
Jeshi la polisi mkoa wa Mwanza bado lipo katika
jitihada kali za kuhakikisha watuhumiwa wote
wanaodaiwa kuhusika katika uhalifu wanakamatwa
na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Kamishina
Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Ahmed Msangi
anawataka wananchi wa jiji na mkoa wa Mwanza
kutulia huku wakiendelea kutoa ushirikiano kwa
jeshi la polisi, ili kuweza kufanya kazi vizuri na
kufanikiwa kuwakamata wahalifu na silaha
wanazotumia mapema na haraka iwezekanavyo.
EATV

Chapisha Maoni

 
Top