Kocha wa Simba, Joseph Omog amesema mazoezi
ya wiki mbili ya kuwajengea na stamina wachezaji
wake yameleta mafanikio aliyotarajia.
Omog alisema kuwa wachezaji wengi wa Simba
walikuwa 'goigoi' kimwili na baadhi hawakuwa na
pumzi za kutosha wakati akiaanza kufundisha
timu.<
Hata hivyo, alisema baada ya programu hiyo,
wachezaji wake wameonekana kuondokana na
tatizo hilo, habari ambayo ni njema kwenye kikosi
chake.
"Wachezaji wamebadilika, tofauti na nilipoanza
kuwafundisha...wengi walitoka kwenye mapumziko
na walirudia wakiwa wameongezeka uzito, lakini
kwa sasa wako vizuri," alisema Omog.
Aidha, alisema amefurahishwa na hali ya wachezaji
kushika haraka maagizo yake, jambo linalompa
imani ndani ya muda mfupi kikosi kitakuwa
kimeimarika.
"Ni kama wiki mbili sasa tuko kwenye mazoezi
Morogoro, nashukuru mambo yanakwenda vizuri
na wachezaji wanashika mafunzo haraka,"
aliongeza Omog.
Kuhusu mechi za kujipima nguvu, Omog - raia wa
Cameroon, alisema watacheza michezo mitatu
kabla ya kuanza vumbi la Ligi Kuu ya Vodacom.
Ligi Kuu inaanza rasmi Agosti 20 na Wekundu hao
wa Msimbazi wampangwa kuanza kucheza dhidi ya
Ndanda FC.
Wakati huo huo klabu ya Simba nafanya
mazungumzo na Azam FC juu ya usajili wa
mshambuliaji Ame Ali 'Zungu'.
Jaffar Iddi Maganga, afisa habari wa klabu ya Azam
FC amethibitisha kuwepo kwa mazungumzo baina
ya klabu yake na Simba juu ya mchezai huyo.
Zungu anaweza kujiunga na Simba wakati wowote
kutegemea na makubaliano yatakayofikiwa baina
ya klabu hizo mbili
Posted Africa News Sports
Chapisha Maoni