0

Klabu ya Medeama ya Ghana imeeleza wazi kuwa
kati ya safu ambayo wanahitaji kujipanga zaidi ni
safu yao ya ulinzi kwa ajili ya kuwadhibiti
mastraika wa Yanga Mzimbabwe, Donald Ngoma
na Mzambia, Obrey Chirwa.
Waghana hao wamekiri kuwa Yanga ni timu nzuri
lakini wamebaini kuwa wanabadilika zaidi pale
mpira unapokuwa kwa mastraika wao hao, hivyo
watajizatiti kuwazuia ili wasiwaletee shida wakiwa
kwao.
“Ni kweli Yanga ni wazuri sehemu nyingi lakini
mastraika wao wawili, yule Ngoma na aliyevaa
namba 7 (Chirwa) ni wazuri sana.
Hao ndiyo tunaotakiwa kucheza nao sana katika
mechi yetu ya marudiano, hatutaki watusumbue,
tukiwazuia hao, tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa,”
alisema straika wa Medeama, Bismark Oppong.
Straika Donald Ngoma alifanikiwa kufunga bao la
kuongoza katika dakika ya pili ya mchezo katika
mechi iliyochezwa hivi karibuni Uwanja wa Taifa,
Dar es Salam kabda ya Bernard Danso wa
Medeama kurudisha bao hilo dakika ya 18



Posted Africa News Sports

Chapisha Maoni

 
Top