0
Mabingwa wa Ligi Kuu ya England Leicester City wamekubaliana na CSKA Moscow kumsajili mshambuliaji kutoka Nigeria Ahmed Musa. Hii ni
kwa mujibu wa wakala wa mchezaji huyo. Musa,
23, alijiunga na CSKA mwaka 2012 na kupachika mabao 54 katika mechi 168. BBC Sport inasema
Leicester 'wamevunja benki' katika ada ya kumsajili mchezaji huyo. BBC Sport pia inasema Musa
alikataa kwenda Southampton, Everton na West Ham. Kocha wa CSKA Moscow Leonid Slusky amekiri kuwa Mnigeria huyo ambaye anaweza
kucheza kama winga au mshambuliaji wa kati,
anaondoka Urusi.

Chapisha Maoni

 
Top