0

TP Mazembe imejiongezea pointi moja
baada ya kupata sare ya bila kufungana
dhidi ya wenyeji wake Mo Bejaia katika
mechi ya Kombe la Shirikisho.
TP Mazembe walikuwa wageni wa Bejaia
katika mechi ngumu usiku wa kuamkia leo
na watakuwa na furaha baada ya kupata
pointi hiyo moja muhimu.
Sare hiyo imeihakikishia TP Mazembe
kufuzu hatua ya nusu fainali kwa asilimia
90 kwa kuwa kama itashinda mechi moja
katika mechi tatu zilizobaki basi itakuwa
ina uhakika wa asilimia 100.
Lakini sare hiyo, imezidi kudidimiza
matumaini ya Yanga kuamka angalau na
kupata pointi zitakazoiwezesha kubadili
mambo kwa kuwa ina pointi moja tu baada
ya kucheza mechi tatu ikipoteza mbili na
kupata sare moja tu dhidi ya Medeama.
TP Mazembe inaendelea kuongoza kundi
hilo ikiwa na pointi saba ikifuatiwa na
Bejaia yenye tano, Medeama ina mbili na
Yanga inaburuza mkia na pointi hiyo moja.




Posted Africa News Sports

Chapisha Maoni

 
Top