Nyota wa timu ya Caps United ya Zimbabwe, Brian
Abbas Amidu, ametua visiwani Zanzibar leo
mchana tayari kabisa kuanza majaribio ya kujiunga
na Azam FC.
Amidu aliyetua nchini jana akitokea Zimbabwe,
mara baada ya kutua visiwani Zanzibar alianza
moja kwa moja mazoezi na wenzake wakati
wakifanya programu maalumu ya kunyoosha
viungo kwenye bwawa la kuogelea ndani ya Hoteli
ya Kitalii ya Mtoni Marine ilipofikia Azam FC.
Mshambuliaji huyo, 26, mwenye uwezo pia wa
kucheza kama kiungo mshambuliaji hakuwa na
maneno mengi ya kusema mara baada ya kuwasili
bali ameweka wazi kuwa yupo tayari kupambana
na kuonyesha kipaji chake ili hatimaye aweze
kufuzu na kusajiliwa.
Amidu anaungana na nyota mwingine wa Kimataifa
wa Zimbabwe, Bruce Kangwa, ambaye bado
anaendelea na majaribio yake akiwa ametimiza
wiki moja hivi leo.
Mbali na kucheza katika kikosi cha Caps United,
Amidu amefanikiwa kucheza soka la kulipwa kwa
miaka minne kabla ya Januari mwaka huu kurejea
nyumbani na kujiunga na Caps.
Usajili wake wa kwanza kucheza kimataifa ilikuwa
ni mwaka 2012 alipojiunga na Kaizer Chiefs ya
Afrika Kusini kisha akapelekwa Black Leopards ya
huko kabla ya Machi mwaka jana kutua Masafi SC
inayoshiriki Ligi Kuu ya Umoja wa Falme za
Kiarabu (UAE).
Wachezaji wengine waliokuwa kwenye majaribio
Azam FC ni washambuliaji Ibrahima Fofana (Ivory
Coast) anayeweza pia kucheza kama winga wa
kushoto pamoja na Mrundi Fuadi Ndayisenga.
Posted Africa News Sports
Chapisha Maoni