0
Neymar amesaini Mkataba mpya na Barcelona
ambao utambakisha hapo hadi Juni 2021
Na una kipengele cha Klabu kulipwa Pauni
Milioni 210 ikiwa atatakiwa na Klabu nyingine
wakati huu wa Mkataba wake.
Neymar, ambae alibakisha Miaka Miwili
kwenye Mkataba wake uliopita, amekuwa
akiripotiwa kutakiwa na Klabu nyingine
ambazo zilitajwa kuwa ni PSG na Manchester
United.
Lakini sasa hayo yatanyamazishwa kwa
Mkataba huu mpya wenye kipengele cha
Barca kulipwa Pauni Milioni 167 ikiwa
atatakiwa na Klabu nyingine ndani ya Mwaka
Mmoja wa wa Mkataba wake huu na Dau hilo
kupanda hadi Pauni Milioni 185 kwa Mwaka
wa Pili wa Mkataba na kufikia Pauni Milioni
210 kwa Miaka Mitatu iliyobaki ya Mkataba.
Neymar, ambae sasa amemaliza Miaka Mitatu
akiwa na Barca, Msimu wa 2015/16
uliokwisha Mei alifunga Goli 31 katika Mechi
49 na kuisadia Barca kutwaa Ubingwa wa La
Liga na Copa del Rey.
Katika Mechi 141 alizoichezea Barca hadi
sasa, Neymar amepachika Mabao 85.
Neymar, ambae hakuichezea Brazil kwenye
Copa America Centenario huko USA Mwezi
uliopita, akipumzishwa ili aichezee Brazil
kwenye Michezo ya Olimpiki itakayofanyika
huko Brazil Mwezi Agosti.

Chapisha Maoni

 
Top