0
Klabu ya Simba imemtambulisha rasmi kocha wao mpya Joseph Omog kama kocha mkuu wa Wekundu wa Msimbazi
Hatimaye dili limekamilika baada ya klabu ya
Simba kufanikiwa kumpata kocha Joseph
Omog kwa kumpa mkataba wa miaka miwili
hadi 2018.
Rais wa Simba Evans Aveva, ameiambia Goal ,
wanafurahi kufikia muafaka huo na wanaimani
kubwa na kocha huyo kwamba atawasaidia
katika mikakati yao ya kuirudisha timu hiyo
kwenye ubora wake uliozoeleka msimu ujao.
“Tunashukuru mimi na viongozi wenzangu
baada ya kufikia makubaliano na Omog,
niimani yetu kwamba atatusaidia na kutupa
mafanikio ambayo tunayatarajia,”amesema
Aveva.
Omog amesema anaujua ukubwa wa Simba na
changamoto zake na amesisitiza atapambana
kuhakikisha kunakuwa na mabadiliko ingawa
amesisitiza suala la muda kwa kuwa kila kitu
hakiwezi kubadilika siku moja.
Kocha huyo amewahi kuifundisha Azam msimu
mmoja uliopita na kuipa timu hiyo ubingwa
wake wa kwanza tangu ilipoanza kushiriki Ligi
ya Vodacom, kabla ya kutimuliwa baada ya
kushindwa kufanya vizuri kwenye michuano ya
Kombe la Shirikisho kwa kutolewa na El
Merreikh ya Sudan kwa mabao 3-2.
Goal.com

Chapisha Maoni

 
Top