winga Andres Townsend kutoka Newcastle United
ambaye amesaini mkataba wa miaka mitano.
Townsend mwenye umri wa miaka ishirini na nne
anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na kocha
Allan Pardew ambaye anakiandaa kikosi chake
kitakachopambana msimu ujao wa ligi kuu ya
England.
Winga huyo aliifungia Newcastle mabao manne
katika mechi kumi na tatu alizocheza tangu atue
klabuni hapo mwezi Januari akitokea Totenham
Hotspurs.
Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa
usajili huo mwenyekiti wa Palace Steve Parish
amesema wanajivunia kupata saini ya nyota huyo
ambaye anaamini uwepo wake kutaboresha kikosi
chao kitakachofanya vizuri kuelekea msimu ujao.
Muingereza huyo aliyesajiliwa kwa dau la pauni
milioni kumi na tatu anatarajia kuwaongezea
washambuliaji Wilfred Zaha na Yannick Bolasie
ambao wamekuwa wakianza katika kikosi cha
kwanza cha timu hiyo.

Chapisha Maoni