marekebisho ya sheria ya kodi ya ongezeko la
thamani ‘VAT’ ya mwaka 2014 kuanzia July 01
2016 kwenye huduma za kifedha kwa kurekebisha
kifungu cha 13 cha jedwali la msamaha wa kodi.
Mamlaka ya mapato Tanzania ‘TRA imetoa
ufafanuzi kuhusu taarifa za upotoshaji kuhusu
marekebisho hayo ya sheria.
Leo July 01 2016 Kamishna mkuu wa mamlaka
ya mapato Tanzania ‘TRA’, Alphayo Kidata
amezungumza na waandishi wa habari na
kusema kuna taarifa ambazo si za kweli
zinazoenezwa kupitia mitandao ya kijamii kuwa
VAT itatozwa kwanye amana ya mwenye fedha
kwenye benki. Hii siyo kweli, ukweli ni kuwa kiasi
cha VAT kitakachotozwa ni asilimia 18 ya kiasi
cha gharama ya huduma iliyotolewa na benki au
taasisi yoyote ya fedha.
Kidata ameeleza mfano huu; Ada ya huduma ya
benki ambayo mteja ametozwa ni sh 1000 kodi
ya ongezeko la thamani itakayotozwa kwenye
kiasi hiki ni sh 152.50 tu na benki kubaki na sh
847.50 kiwango hicho cha sh 152.50 ndicho
kitakachorejeshwa serikalini na benki au taasisi
ya fedha baada ya kupunguza kodi ya ongezeko
la thamani iliyolipwa kwenye manunuzi ambayo
yamefanywa na benki au taasisi ya fedha husika.
TRA imezitaka benki na taasisi za fedha
zilizoamua kwa makusudi kutoa taarifa
zisizosahihi kwa umma kuacha mara moja
vinginevyo hatua kali zitachukuliwa.
Aidha imeziagiza benki na taasisi zinazohusika
kurekebisha mara moja taarifa
walizokwishazisambaza ili zibebe maudhui sahihi
ya marekebisho ya sheria hii.
Chz
Mpekuzi blog

Chapisha Maoni