anasema kuwa alienda nchini Uingereza
kuthibitisha kuwa inawezekana kucheza mchezo
mzuri katika ligi ya Uingereza.
Gurdiola mwenye umri wa miaka 45 ambaye
ametia kandarasi ya miaka mitatu ,amesema kuwa
alipendelea kusalia kuifunza Bayern Munich ,lakini
alitaka mtihani mwengine katika ukufunzi wake.
Raia huyo wa Uhispania amekiri kwamba alikuwa
na kila alichohitaji wakati alipokuwa Barcelona
,lakini akakana kuwa huenda anakabiliwa na
kibarua kigumu katika klabu ya Manchester City.
''Niko hapa kuthibitisha kuwa ninaweza
kuchezesha soka nzuri vilevile nimekuwa
nikicheza'',alisema.
Alipoulizwa iwapo anaweza kuanzisha mtindo
mzuri wa tiki-taka kama ule wa Barcelona ,alisema
Guardiola:''Hiyo ndio sababu niko hapa''.
Aliongezea:''Sijawahi kucheza wakati wa siku kuu
ya Boxing Dei.Sijawahi kuwa katika uwanja wakati
ambapo kuna upepo mkali na baridi na uwanja sio
mzuri.Ni lengo langu.Nataka kuwathibitishia''.
Chapisha Maoni