0
Sakata la usajili wa kiungo Mfaransa Paul Pogba limeingia katika hatua nyingine baada ya Real
Madrid kushindwa kukataa kama hawamuhitaji mchezaji huyo.
Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane amekataa kuthibitisha kwamba wana mpango wa kumsajili Pogba.
Man United ndiyo timu inayotajwa mno kumwania
Pogba huku wakipandisha dau lao toka paundi milioni 86 mpaka paundi milioni 92 wakitarajia kumlipa paundi 200,000 kwa wiki.
Pogba ambaye inasemekana anaihusudu vilivyo
Real Madrid yawezekana tukasikia ametimkia Real Madrid na hii pengine itachangiwa na uwepo wa
Zidane katika kikosi cha Madrid japokua taarifa zingine zinadai kwamba Man United wameshamalizana na Pogba.

Chapisha Maoni

 
Top