0
Kumekuwa na taarifa maalum zikisema
kuwa Shirikisho la Soka Uingereza (FA)
limepanga kuziruhusu timu za nchi hiyo
kuanza kuwatumia wachezaji wanne
wakati wa dakika 30 za nyongeza
kwenye hatua ya robo fainali ya kombe
la FA msimu ujao wa michuano hiyo.
Mashindano hayo ya kombe la FA
yanatarajiwa kuanza hapo Agosti 5
mwaka huu huku yakizishirikisha timu
za ligi kuu ya Uingereza na zile zilizopo
kwenye daraja la kwanza. Sheria hiyo ya
kuwabadilisha wachezaji wanne kwa
mara ya kwanza iliweza kujaribiwa
kwenye mashindano ya Copa America
yaliyomalizika mwezi Juni, 2016.
Pia, sheria hiyo inatarajiwa kupitishwa
na chombo chenye mamlaka ya kubadili
Sheria za Soka (IFAB-International
Football Association) ili iweze kutumika
pia mpaka kwenye michuano yote
iliyokuwa chini ya FIFA ikiwemo Kombe
la Dunia na mingineyo mingi. Sheria hii
mpya itatumika kuanzia robo fainali za
FA Cup.
Maamuzi haya pia ni sambamba na yale
mabadiliko ya kufuta mechi za
marudiano endapo timu zitaenda sare
kuanzia robo fainali. FA Cup itaanza
Agosti 5 kwa mechi 184 za raundi za
awali ambazo hazishirikishi timu za Ligi
Kuu Uingereza na zile za daraja la chini
yake Championship, mabadiliko
makubwa yanatarajiwa kutokana na hili.

Chapisha Maoni

 
Top