0

Mkwasa ameita kikosi cha wachezaji 24
watakaoanza kambi kuajindaa na mchezo wa
kufuzu faInali za Mataifa ya Afrika AFCON dhidi ya
Nigeria utakaopigwa Lagos, Septemba 2
Kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’
Boniface Mkwasa ameita kikosi cha wachezaji 24
watakaoanza kambi kuajindaa na mchezo wa
kufuzu faunali za Mataifa ya Afrika AFCON dhidi
ya Nigeria utakaopigwa Lagos, Septemba 2,
2016.
Mkwasa ameiambia Goal , amefanya mabadiliko
makubwa kwenye kikosi hicho kwa kuwaacha
baadhi ya wachezaji akiwemo nahodha Mbwana
Samatta, kwasababu mchezo huo hawaupi
umuhimu mkubwa kutokana ni wakukamilisha
ratiba baada ya timu hizo mbili tayari imepoteza
nafasi ya kufuzu fainali hizo za Gabon.
“Nimetoa nafasi kwa vijana wengi ili waweze
kutoa mchango wao kwa taifa kwa sababu
pamoja kwamba hatuna nafasi lakini hatupo tayari
kupoteza mchezo huo kwasababu tunataka
heshima hasa ukizingatia wenzetu Nigeria nao
wana benchi jipya la ufundi na kwasababu
wameshuka kwenye viwango vya FIFA, watataka
kutufunga ili kurudisha heshima yao,”amesema
Mkwasa.

Wachezaji walioitwa
Makipa;
Deogratius Munishi Yanga, Aishi Manula Azam na
Benny Kakolanya Prisons.

Mabeki;
Kelvin Yondani Yanga, Aggrey Morris Azam,
Oscar Joshua Yanga, Mohamed Husein ‘Zimbwe’
Simba, Juma Abdul Yanga na Erasto Nyoni
Azam.

Viungo:
Himid Mao, Mohamed Ibrahim, Shiza Kichuya,
Jonas Mkude, Ibrahim Jeba, Mwinyi Kazimoto,
Farid Mussa, Juma Mahadhi na Hassan Kabunda,

Washambuliaji
Simon Msuva, Joseph Mahundi, Jamal Mnyate,
Ibrahim Ajib, John Bocco na Jeremia Juma.



Posted Africa News Sports

Chapisha Maoni

 
Top