0
Klabu ya soka ya Real wanaanza
mazoezi Jumamosi na hii ni mara ya
kwanza kwa kocha wao Zinedine Zidane
kuiongoza timu katika matayarisho ya
kabla ya msimu mpya. Lakini hatakuwa
na kikosi kamili kwani baadhi ya nyota
wake bado wako mapumzikonI.
Baada ya kushiriki michuano ya
kimataifa ya Euro 2016 na Copa America
Centenario, watakaokosekana ni pamoja
na nyota wao mkubwa Cristiano Ronaldo
ambaye aliiongoza nchi yake kutwaa
Ubingwa wa Ulaya.
Wachezaji akina Keylor Navas, Kiko
Casilla, Ruben Yanez, Dani Carvajal,
Danilo, Raphael Varane, Casemiro,
Nacho, Marcelo, Jese, Marco Asensio,
Isco na Karim Benzema watakuwepo
mazoezini. Jana, Real watasafiri kwenda
Canada kupiga kambi na kisha kuelekea
Marekani kucheza michuano ya
International Champions Cup.
Klabu ya Real wamepanga kucheza
mechi 3 tu za kujipima kwani hapo
Agosti 9 wapo huko Trondheim, Norway
kucheza na mabingwa wa UEFA EUROPA
LIGI Sevilla kuwania UEFA Super Cup.
RATIBA YAO:
Julai 28: Real Madrid – Paris Saint-
Germain (Ohio Stadium, 15:30 Mchana)
Julai 30: Real Madrid – Chelsea
(Michigan Stadium, 23:00 CET)
Agosti 4: Real Madrid – Bayern Munich
(Metlife Stadium15:30 CET)
Agosti 9: UEFA Super Cup, Real Madrid
– Sevilla (Lerkendal Stadion, 23:45 CET)

Chapisha Maoni

 
Top