amezidi kuonyesha makali yake nchini
Ubelgiji baada ya kuifungia KRC Genk bao muhimu lililoipa ushindi wa mabao 2-1
dhidi ya Oostende. Karelis ndiye alikuwa wa kwanza kufunga upande wa Genk, ilikuwa ni katika dakika ya
50, Samatta akaongeza katika dakika ya
90+1, yaani katika ile dakika moja ya
nyongeza.
Bao hilo la Samatta limekuwa lililoibeba
Genk kwa kuwa, Musona aliifungia
Oostende bao dakika 90+3 ikiwa ni ya
mwisho kabisa baada ya kuongezwa dakika tatu.
Kama ingekuwa bado wanaongoza kwa bao moja la Karelis, maana yake Genk
wangeambulia sare ya bao 1-1 baada ya
dakika 90.
Chapisha Maoni