Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji amesema
hatambui lolote kuhusiana na kufungiwa kwa Muro
ambaye ni Mkuu wa Habari na Mawasiliano wa
klabu hiyo kongwe zaidi nchini.
Akizungumza na mtandao wa SALEHJEMBE, Manji
amesema klabu hiyo inaendelea kumtambua Muro
kama mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano
na anaendelea kufanya kazi zake kama kawaida.
“Kama taarifa tumesikia kwenye magazeti na redio,
kweli taasisi kama Yanga, msemaji wake
anasimamishwa kwa njia hiyo.
“Hao waliomsimamisha pia ni taasisi, vipi wafanye
hivyo. Yanga tunawezaje kuamini hilo? Muro bado
yuko kazini na anaendelea na shughuli zake kama
kawaida,” alisema Manji.
Manji amesisitiza, kuwa kama ni kweli basi TFF
inapaswa kutoa hukumu ya kumfungia Muro kama
ambavyo wamekuwa wakisikia.
TFF kupitia kamati ya nidhamu ilitangaza
kumfungia Muro mwaka mmoja ikiwa ni pamoja na
kumpiga faini.
Lakini imekuwa ikisita kutoa hukumu yake
inayohusiana na Muro, jambo ambalo linaifanya
Yanga kuona kuna upotofu wa mambo na
kukiukwa kwa usahihi.
Hukumu ya Muro imekuwa ni kitu cha uficho licha
ya kamati hiyo chini ya TFF kumhukumu, jambo
ambalo linaonekana ni kichekesho.
Posted Africa News Sports
Chapisha Maoni