0

Mkutano mkuu wa klabu ya Simba umemalizika
katika ukumbi wa Maofisa wa Polisi Dar es
Salaam huku uongozi na wanachama
wakishindwa kuelewana kuhusu swala la
kumkabidhi timu Mo
Mkutano mkuu wa klabu ya Simba umemalizika
katika ukumbi wa Maofisa wa Polisi Dar es
Salaam huku uongozi na wanachama
wakishindwa kuelewana kuhusu swala la
kumkabidhi timu Bilionea Mohamed Dewji MO.
Goal ikuwepo kwenye mkutano huo na
kushuhudia wanachama wengi waliojitokeza
walionekana kuwa na jamb moja tu yakupitisha
agenda kuu kuwa mabadiliko ya mfumo wa
umiliki wa klabu kutoka uanachama wa kawaida
kwenda kwenye mfumo wa hisa.
Rais wa Simba alisimama na kusema uongozi
uliteua kamati kukusanya maoni kwa wadau,
wanachama na wapenzi kuhusu suala la mfumo
wa hisa.
Kamati hiyo ilitoa mapendekezo ya awali ya
kutaka mfumo wa hisa lakini imeomba muda
zaidi kutoa ripoti na mapendekezo ya mwisho.
Hata hivyo wanachama walipinga kwa sauti na
kudai muda waliopewa umetosha na wanataka
mabadiliko tu.
Mkutano ulimalizika kwa mwenyekiti wa kamati
ya maoni kushindwa kuendelea baada ya
wanachama kuingilia hotuba yake na hivyo
kumlazimu Rais Aveva kusimama na kumaliza
mkutano kwa staili ya pekee.
Kilichoonekana ni uongozi kukubali agenda ya
mabadiliko lakini wanasubiri ripoti ya mwisho ya
kamati iliyoteuliwa kukusanya maoni ya suala la
mfumo wa hisa.



Posted Africa News Sports

Chapisha Maoni

 
Top