Timu ya taifa ya vijana
chini ya miaka 17
Serengeti boys hii leo
wameibuka na ushindi wa
goli 6-0 mbele ya
mashabiki wa Shelsheli
katika mchezo wa
marejeano kusaka tiketi ya
kushiriki mataifa ya Afrika
kwa vijana chini ya miaka
17.
Katika mchezo wa leo
uliochezwa nchini
Shelisheli Serengeti Boys
walikwenda mapumziko
wakiwa mbele kwa goli
2-0, ambapo goli la
kwanza lilifungwa katika
dakika ya 9 kupitia
Ibrahim Abdallah
aliyemalizia mpira
uliotemwa na kipa wa
Shelisheli kufuatia shuti la
Asad Juma.
Asad Juma aliiandika
Serengeti boys goli la tau
katika dakika ya 50 kabla
ya Issa Mwakamba
kufunga goli la 4 katika
dakika ya 61.
Saad Juma aliiandikia
Serengeti boys goli la
tano katika dakika 70
kabla ya kupata goli la 6
na kupelekea mchezo
kumalizika kwa Serengeti
boys kuibuka na ushindi
wa goli 6-0.
Kwa matokeo hayo ya leo
Serengeti boys
wamewatoa Shelisheli kwa
matokeo ya jumla ya goli
9-0, na sasa watakutana
na Sauzi Afrika katika
hatua inayofuata ya
kusaka tiketi ya kwenda
Madagascar mwakani
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.