0

Kampuni ya mashindano ya bahati nasibu
inayodhamini Ligi Kuu ya Kenya imetia saini
mkataba wa kuwa mdhamini wa klabu ya Hull City
ya Uingereza.
Kampuni hiyo ya SportPesa, ambayo huandaa
mashindano ya kubashiri matokeo ya mechi nchini
Kenya, imetia saini mkataba wa kudhamini Hull
City kwa misimu mitatu.
Klabu ya Hull City ilifanikiwa kurejea kwenye Ligi
ya Premia msimu utakaoanza mwezi ujao.
Hull City watafungua msimu kwa mechi ya
nyumbani dhidi ya mabingwa Leicester City.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa klabu hiyo,
udhamini wa SportPesa ndio wa juu zaidi kuwahi
kupokelewa na klabu hiyo katika historia yake ya
miaka 112.
Hull City imekuwa ikidhaminiwa na kituo cha
burudani cha Flamingo Land.



Posted Africa News Sports

Chapisha Maoni

 
Top