ujumbe kwa Spika wa Bunge Job Ndugai kuomba
kuyakutanisha makundi mawili yanayosigana
bungeni ili kuleta muafaka wenye tija kwa taifa.
Mwenyekiti wa taasisi hiyo Sheikh Sadick
Godigodi jana alisema kumeguka kwa Bunge
kunakosababishwa na Kambi ya Upinzani kuona
inaonewa na maamuzi ya Naibu Spika, Dk. Tulia
Akson kunahitaji viongozi wa dini kuingilia kati na
kupata suluhu.
"Tunatarajia katika Bunge lijalo litakaloanza
Septemba kuwasilisha ujumbe kwa Spika ili
tupewe nafasi ya kutatua mgogoro huu kwa
maana wabunge wote wanatakiwa kuwepo
bungeni kuwakilisha matatizo ya wananchi,"
alisema Sheikh Godigodi.
"Haiwezekani kundi moja likawa nje na jingine
likaendelea, tunahitaji maridhiano ya pande zote
mbili za muhimili huo.”
Kambi ya Upinzani Bungeni ilisusia vikao vya
Bunge la Bajeti kwa zaidi ya siku 70 kupinga kile
kilichoita kuburuzwa na
Naibu Spika katika uendeshaji wa chombo hicho
cha kutunga sheria.
Kambi hiyo, ilianza kutoka nje Mei 30 baada ya
Naibu Sika kukataa hoja ya Mbunge wa Arumeru
Mashariki, Joshua
Nassari (Chadema), ya kutaka Bunge likatize
shughuli zake na kujadili hoja ya kufukuzwa kwa
wanafunzi zaidi ya 700 wa Chuo Kikuu cha
Dodoma (Udom).
Ingawa kitendo hicho cha Naibu Spika kiliwaudhi
wabunge wa chama tawala (CCM) na Upinzani,
kambi hiyo haikurudi ndani mpaka Bunge
lilipoahirishwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
katikati ya wiki iliyopita.
Mshauri wa mambo ya kisheria na kidiplomasia
wa taasisi hiyo ya Maridhiano, Agustino Matefu
alisema mbali na kusuluhisha migogoro chochezi
ya kidini kwa kutoa elimu sahihi kwa umma, pia
wamejikita katika kusuluhisha migogoro sugu kati
ya wakulima na wafugaji nchini.
“Tumetoa mchango mkubwa wa kuleta suluhu ya
migogoro ya ardhi baina ya wafugaji na wakulima
mkoani Morogoro katika wilaya za Mvomero,
Kilombero na Kilosa (na) ndio maana watanzania
wanaona hali ni kama sasa imekuwa shwari,”
alisema Matefu.
Matefu alisema wamepata mualiko rasmi kwa
uongozi wa Mkoa wa Iringa na wanatarajia
kwenda huko baada ya uzinduzi rasmi wa taasisi
hiyo utakaofanyika Julai 13 jijini Dar es Salaam.
Katibu wa taasisi hiyo, Mchungaji Oswald Mlay
alisema kuwa uzinduzi na utambulisho wa taasisi
hiyo utaendana na utoaji tuzo ya amani kwa
viongozi na watu mbalimbali waliojitoa
kuhamasisha udumishwaji wa amani nchini.
Wanaotarajiwa kupewa tuzo ni Mama Maria
Nyerere kwa niaba ya Hayati Baba wa Taifa,
Mwalimu Nyerere ambae atatunukiwa tuzo ya
Amani uasisi wa amani ya taifa.
Chapisha Maoni