
Mchezaji huyo kutoka Armenia atagharimu takriban pauni milioni 26 (Daily Mail), Manchester City wapo
tayari kulipa hadi pauni milioni 50 kumsajili beki
John Stones, 22, kabla ya kuanza kwa mechi za kabla ya msimu (Telegraph), Crystal Palace wamekubali kulipa pauni milioni 12.5 kumsajili beki wa West Ham James Tomkins, 27 (Daily Mail),
mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wanafikiria kumsajili beki wa kati wa Arsenal, 30, ambaye
mkataba wake Emirates unamalizika mwaka 2019 (Evening Standard),
Everton wamekubali kumsajili kiungo wa Ubelgiji Axel Witsel, 27, kutoka Zenith St Petersburg na
watamlipa mchezaji huyo zaidi ya pauni 100,000
kwa wiki (Squawka), Stoke City wametoa dau la pauni milioni 16 kutaka kumsajili mshambuliaji wa
West Brom, Saido Berahino, 22, na wako tayari kumlipa pauni 70,000 kwa wiki (Mirror).
Burnley wanataka kumfanya beki Michael Keane, 23, kuwa mchezaji anayelipwa zaidi katika historia
ya klabu hiyo ili kuzuia kusajiliwa na Leicester City
(Mirror), mchezaji wa zamani wa Arsenal na Manchester United Robin van Persie, 32, anauzwa na klabu yake ya Fernabahce (Evening Standard),
mshambuliaji wa Manchester United Ashley Fletcher, 20, amekataa mkataba mpya na atafanya vipimo West Ham (Manchester Evening News).
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.