
ya jezi yake (Daily Telegraph), Manchester United
wanajiandaa kumsajili mshambuliaji wa Pachuca, Hirving Lozano, 20, atakapotoka kwenye michuano
ya Olimpiki akiichezea timu yake ya taifa ya Mexico
(Futbol Entre Lineas), Crystal Palace huenda wakamuuza Mkongomani Yannick Bolasie, 27, na
West Ham wanataka kumsajili winga huyo (Daily
Mirror), winga wa Dinamo Zagreb, Marko Pjaka, 21, ana nafasi kubwa ya kuhamia katika EPL msimu ujao, kwa mujibu wa mkurugenzi wa michezo wa
klabu hiyo ya Croatia. Liverpool wanamtazama
mchezaji huyo (FC Internews), meneja mpya wa Manchester City Pep Guardiola bado anamtaka beki wa kati wa Everton John Stones, 21, licha ya klabu
yake kutaka pauni milioni 50 (Daily Mail), kiungo wa Derby County, Will Hughes, 21, anatazamwa na
Manchester United, wakati meneja mpya Jose Mourinho akitaka kuongeza idadi ya wachezaji
wazawa katika kikosi chake (Sun), meneja wa Everton Ronald Koeman anataka kumsajili kipa wa
Valencia Diego Alves, 31, msimu huu (Deporte Valeciano), Manchester City wanajiandaa kumsajii
kipa Geronimo Rulli, 24, kutoka Deportivo Maldonado ya Uruguay kwa pauni milioni 7.5, ili
kuleta ushindani kwa Joe Hart (Express), kiungo mshambuliaji wa Real Madrid James Rodriguez,
24, anajiandaa kujiunga na Paris St-Germain
(Yahoo Sports France), Liverpool wanasema kiungo wao Joe Allen, 26, ana thamani ya pauni milioni
14. Swansea wametoa pauni milioni 8 wakimtaka mchezaji huyo aliyebakiza mwaka mmoja kwenye
mkataba wake (Daily Mail), kusajiliwa kwa Michy Batshuayi, 21, na Chelsea huenda kukamfanya
Diego Costa, 27, kuondoka Darajani (Daily
Telegraph), winga wa Manchester United Adnan Januzaj, 21, atamwambia Mourinho kuwa anataka kuondoka iwapo hayupo kwenye mipango yake ya
kikosi cha kwanza (Sun), beki wa zamani wa Real Madrid Alvaro Arbeloa, 33, anasakwa na Newcastle
United (Football Espana), meneja wa zamani wa
Chelsea Guus Hiddink anataka kuzungumza na chama cha soka cha England FA, kuchukua mikoba
ya Roy Hodgson (The Times), meneja mpya wa Chelsea, Antonio Conte anamtaka mshambuliaji wa
Southampton, Graziano Pelle, 30, (Sky Italia), mshambuliaji wa Everton Romelu Lukaku, 23, anataka mazungumzo mapya na klabu hiyo baada
ya mmiliki mpya Farhad Mori kusema mchezaji huyo ana thamani ya pauni milioni 75 (Daily Star),
mchambuliaji wa Manchester City Kelechi Iheanacho, 19, amekiri kuwa hatokwenda kwenye
michuano ya Olimpiki baada ya klabu yake kuweka
pingamizi kwa Nigeria kumuita (ESPN), na Liverpool wako tayari kumuacha kipa kutoka Hungary, Adam Bogdan aondoke, na kujunga na
Wigan Athletic (Daily Star).
Chapisha Maoni