0

KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), Selestine Mwesigwa
amewaasa makocha waliohitimu kozi ya
ukocha ya leseni B kutumia taaluma
waliyoipata ipasavyo.
Mwesigwa aliyasema hayo juzi
alipofunga kozi ya siku 16 iliyokuwa
ikifanyika kwenye Uwanja wa Karume,
Dar es Salaam ambayo ilihudhuriwa na
makocha 29 kutoka mikoa mbalimbali ya
Tanzania.
“TFF tunafurahi kuwa na idadi kubwa ya
makocha wa ngazi ya juu hivyo nawasihi
msiende kuweka vyeti ndani bali
mkafundishe soka ili kuibua vipaji na
soka letu likue,” alisema Mwesigwa.
Pia Mwesigwa aliwapongeza wahitimu
hao kwa kufanya vizuri kwani baadhi yao
wanafundisha timu za taifa, Ligi Kuu na
daraja la kwanza na timu zao
zimeonesha ushindani kwenye soka.
Baadhi ya makocha ambao wanafundisha
timu hizo ni Bakari Shime (Timu ya taifa
ya vijana chini ya umri wa miaka 17-
Serengeti Boys), Edna Lema (Timu ya
soka ya taifa ya wanawake Twiga Stars),
Zuberi Katwila (Mtibwa Sugar), Athuman
Bilal (Stand United) Salvatory Edward
(African Lyon) Maalim Salehe (Ashanti
United) Nico Kiondo (Simba B).
Naye mkufunzi wa kozi hiyo Salum
Madadi aliwapongeza wahitimu kwani
wameonyesha moyo wa kujifunza na
walijitolea kuhakikisha wanafanya vizuri
hata pale ambapo walikuwa wamechoka.
Baada ya kufungwa kwa kozi hiyo ya
leseni B, leo inatarajiwa kuanza kwa kozi
nyingine ya leseni A itakayokuwa
inafanyika hapo hapo TFF, Karume Ilala.



Posted Africa News Sports

Chapisha Maoni

 
Top