KOCHA Mkuu wa Mtibwa Sugar, Salum
Mayanga amefurahia ujio wa mchezaji
Haruna Chanongo kwenye kikosi chake.
Akizungumza na gazeti hili juzi,
Mayanga alisema kuwa kiungo Chanongo
amekuja wakati sahihi baada ya
wachezaji kadhaa kuondoka kwenye
kikosi hicho cha wakata miwa wa Turiani
Manungu.
“Timu yetu imeondokewa na wachezaji
wengi na kwa sasa ndio tunaanza
kujenga kikosi upya hivyo kumpata
Chanongo ambaye ana uzoefu itasaidia
kuimarisha timu,” alisema Mayanga.
Chanongo amesaini mkataba wa miaka
miwili kuichezea timu hiyo ya Manungu,
Morogoro akitokea Stand United ya
Shinyanga.
Wachezaji ambao wameondoka baada ya
msimu kumal izika ni winga Shiza
Kichuya, Ibrahim Mohamed na Mzamiru
Yasini waliosajiliwa Simba na Vicent
Andrew aliyesajiliwa Yanga.
Mtibwa Sugar ambayo imekuwa haifanyi
vizuri katika misimu ya karibuni ya Ligi
Kuu imeanza mazoezi Dar es Salaam
kwa ajili ya kujiandaa na msimu wa
mwaka 2016/2017.
Posted Africa News Sports
Chapisha Maoni