ambayo kambi ya upinzani itayafanya endapo wataitwa na kamati ya maridhiano juu ya kususia
Bunge wao watakachoangalia ni maslahi ya kitaifa.
Injinia Mbatia ameyasema hayo alipofanya mahojiano maalumu na kipindi cha EA Radio Jijini
Dar es salaam kuhusu hoja ya wao kukutanishwn na kamati ya maridhiano kujadili kitendo chao cha
kususia bunge la bajeti.
''Sisi kabla ya kufanya jambo lolote tunaangalia
mama Tanzania kwanza, swala la maridhiano
limekuwa jambo letu mara zote , tangu tumeanza
masuala ya katiba pamoja na mambo ya
demokrasia tuna'' amesema Mbatia.
''Sisi hatujadili mtu tunajadili mfumo, Bunge kwa
mujibu wa katiba linatakiwa lisimamie serikali na
kuishauri kwa kuheshimu utu na kuhakikisha yale
tunayoyafanya yanakuwa na maslahi ya taifa''-
Amesema Mbatia.
Mgogoro wetu na Naibu Spika ni kwamba
anaongoza Bunge kwa kuagizwa na serikali na hii
itaonekana wazi kwamba hoja ya maslahi ya
wabunge wabunge wa CCM waliosema hapana
walikuwa ni wengi na walikuwa wao kwa wao lakini
akasema anatumia kura ya veto hivyo hoja hiyo
imepita.
Mbatia amehitimisha kwa kusema watanzania
wategemee kama hali ya maridhiano haitapatikana
wategemee mambo hayohayo ya kususia mambo
kurudi kwenye jamii mfano tuu suala la VAT
serikali imeshindwa kulifafanua kwa kuwa waziri
amesema la kwake gavana wa benki akasema la
kwake na mkurugenzi wa tra akasema la kwake.
Chapisha Maoni