MAREKANI, baada ya mtu mwingine mwenye asili ya AFRIKA kuuawa kwa makusudi na askari
aliyemfyatulia risasi, huko MINESOTA.
Rafiki wa kike wa mtu huyo, alirekodi tukio hilo
kupitia kwenye simu yake ya mkononi na
kulisambaza katika mitandao ya kijamii.
Mwanamke huyo anasema askari Polisi mzungu
alimfyatulia risasi rafiki yake wa kiume alipokuwa
akimuonyesha leseni yake ya kuendeshea gari
baada ya kusimamishwa na polisi.
Polisi huyo alimfyatulia risasi, akiwa ndani ya gari
lake, pamoja na rafiki yake huyo na mtoto wao
mdogo wa kike.
Amesema askari huyo alikasirishwa baada ya
marehemu kumweleza kuwa alikuwa akimiliki
silaha. Rafiki yake huyo anasema marehemu
alikuwa na leseni ya kumiliki silaha hiyo.
Wakati huo huo, kumekuwa na maandamano
makubwa katika jimbo la LOUISSIANA nchini
MAREKANI, baada ya askari Polisi wawili kumuua
mtu mmoja mwenye asili ya AFRIKA, nje ya duka
moja.
Mmiliki wa duka hilo alichukua picha ya video
iliyoonyesha tukio hilo na kuisambaza kwenye
mitandao ya kijamii. Polisi wawili wa kizungu
wameonekana wakimkandamizi chini mtu huyo,
ambaye hakuwa na silaha, kisha kumfyatulia risasi
kadhaa kifuani na kusababisha kifo chake.
Watu wenye asili ya AFRIKA wamelitaka shirika la
upelelezi la MAREKANI kuchunguza tukio hilo na
kuchukua hatua.
Tayari jeshi la Polisi nchini MAREKANI, limewapatia
likizo askari waliohusika na tukio hilo ili kupisha
uchunguzi kuhusiana na mauaji hayo.
Chapisha Maoni