0
Mili saba kati ya tisa waliokufa mto Ruvuma Julai 2 mwaka huu baada ya mtumbwi waliopanda kupinduka baada ya kugonga kingo za Mto huo
wakati wakitoka mnadani Mkenda Songea wakivuka
mto Ruvuma kuelekea Nyasa mkoani Ruvuma
imepatikana katika mto huo.
Kulingana na ITV, Afisa Tarafa ya Mpepo wilayani
Nyasa mkoani Ruvuma Simon Beebwa amesema
miili hiyo ni pamoja na wa mama mjamzito Hadija
Said (41) na miili mingine ni Omary Jela
(11),Fadhili hamis (8) na Zurufa Ally (14),Awetu
Mohamed (14),Omary Waziri(13) na Sttumai
abdalah mtoto wa miezi mitano.
Amesema kuwa miili hiyo imepatikana baada ya
kupelekwa boti kutoka Ziwa Nyasa wilayani Nyasa
ya kusaidia kutafuta miili hiyo na kwamba hadi
sasa imebakia miili miwili ambayo bado
haijapatikana na kwamba juhudi za kuitafuta miili
hiyo zinaendelea.

Chapisha Maoni

 
Top