Wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye michuano ya Kimataifa Yanga ambao wanashiriki kombe la shirikisho barani Afrika hatua ya makundi
wamechapwa mabao 3-1 na Medeama ya Ghana.
Kichapo hicho 'kitakatifu' kimefuta ndoto za klabu hiyo ya mtaa wa Jangwani iliyokuwa inahitaji kupata ushindi katika mchezo huo ili iendelee
kupigania nafasi ya kutinga nusu fainali.
Safu ya ulinzi ya klabu ya Yanga imeendelea kufanya uzembe na kuruhusu mabao 'mepesi'.
Aidha pengo la Vicent Boussou ambaye anatumikia adhabu ya kadi za njano limeoonekana wazi.
Nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro' amecheza nafasi ya Boussou.
Yanga sasa imebaki na michezo miwili ya kukamilisha ratiba dhidi ya Mo Bejaia na TP Mazembe.
Hakika itahitaji kufanya marekebisho makubwa ili iweze kufanya vyema kwenye michuano ya
Kimataifa mwakani.
Bado inaburuza mkia kundi A ikiwa na alama moja pekee wakati Medeama imeweka hai matuamini ya
kutinga nusu fainali baada ya kufikisha alama tano sawa na Mo Bejaia iliyo nafasi ya pili.
TP Mazembe itachuana na Mo Bejaia ambapo kama ikipata ushindi itakuwa imekaribia kufuzu hatua ya nusu fainali.
Posted Africa News Sports
Chapisha Maoni