0

Kipa nyota nchini, Juma Kaseja ameteuliwa kuwa
kocha wa makipa wa kikosi cha vijana chini ya
miaka 17, Serengeti Boys.
Kaseja anaungana na kikosi hicho ambacho
kinasafiri kwenda kambini Madagascar kupitia
Afrika Kusini.
Kaseja amechukua nafasi ya kocha wa makipa
aliyekuwepo awali ambaye anabaki nchini kwa ajili
ya kushiriki kozi za ukocha.
Kipa huyo wa zamani wa Simba, alikuwa katika
mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya na
Mbeya City.



Posted Africa News Sports

Chapisha Maoni

 
Top