0

Mjumbe wa ngazi ya juu wa Kamati ya Olimpiki
Patrick Hickey amewekwa chini ya ulinzi kwa
kuhusishwa na ufisadi wa tiketi za Olimpiki.
Afisa huyo amejiuzulu kwa muda ili kupisha
uchunguzi baada ya kuwekwa chini ya ulinzi kwa
kuuza tiketi kinyume cha sheria.
Kumekuwa na uhudhuriaji mdogo katika michezo
ya olimpic huko Rio ni kutokana na tiketi kuuzwa
na baadhi ya maafsa kwa bei ya juu sana
kimagendo.
Kukamatwa kwa Patrick Hickey, mmoja wa
viongozi wa juu wa michezo ya Olympic ya ulaya,
bado ni hoja kubwa kwa makao makuu ya polisi ya
Brazil, kufuatia kukwamatwa kwa viongozi hao
kumehusishwa kampuni ya kimataifa ya usimamizi
wa michezo, THG.
Zaidi ya tiketi elfu moja za michezo ya olimpic
zimesitishwa, ikiwemo tiketi za ufunguzi na zile za
mbio za riadha, na wachunguzi wanasema madai
ya udanganyifu yangeweza kutengeneza zaidi euro
milioni mbili.
Kampuni hiyo ya kusimamia michezo ya kimataifa
imekanusha shutma hizo huku jaji wa Brazil wiki
hii akitoa agizo la kukamatwa washukiwa zaidi
waliohusika na kesi hiyo.



Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

 
Top