0

Brazil wametinga Fainali wakiwania Medali
yao ya Kwanza kabisa ya Michezo ya Olimpiki
baada ya kuwatwanga Honduras Bao 6-0.
Brazil walianza Mechi hii kwa kishindo kikubwa
pale Kepteni wao Neymar alipofunga Bao lao la
kwanza baada ya Sekunde 14 tu tangu Mechi
ianze ikiwa ni Historia kwa Olimpiki kwa Bao la
haraka kiasi hicho.
Hata hivyo Neymar alileta kutaharuki Uwanjani
baada ya kuumia akifunga Bao hilo alipogongana
na Kipa Luis Lopez na kutolewa nje kwa Machela.
Neymar aliweza kurudi tena Uwanjani lakini muda
mfupi baadae akakaa chini kwa maumivu na
kutolewa tena nje lakini akaweza kurudi tena na
kuendelea tena na Mechi.
Brazil waliongeza Bao 2 katika Dakika za 26 na 35
kupitia Gabriel Jesus.
Hadi Mapumziko Brazil 3 Honduras 0.
Kipindi cha Pili Brazil walipiga Bao 3 nyingine za
Dakika za 51, 79 na 90 ambalo lilikuwa la Penati.
Bao hizo zilifungwa na Marquinhos, Luan na
Neymar kwa Prnati.
Brazil sasa watacheza Fainali na Mshindi kati ya
Nigeria na Germany ambao wanacheza baadae
Leo.



Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

 
Top