0

Mbwana Samatta jana
usiku alifunga bao moja kati ya mabao mawili
waliyopata KRC Genk ugenini huko Russia.
Genk ikiwa ugenini ikicheza na wenyeji Locomotiv
Zagreb ilipata sare ya bao 2-2 katika mchezo wa
kwanza wa hatua ya mwisho ya mtoano katika
michuano ya Europa League.
Kiungo Leon Bailey alitangulia kuipatia Genk bao
la kwanza kwa njia ya penati kisha Samatta
akafunga la pili dakika chache baada Mapumziko,
Genk wakiwa na goli moja mpaka mapumziko.
Wenyeji walicharuka na kurudisha magoli yote
mawili kupitia kwa Mirko Malik na Ivan Fiolic
dakika ya 52 na dakika ya 59 na kufanya mchezo
huo kumalizika kwa sare hiyo.
Mchezo wa marudiano utakua wiki ijayo ambapo
Genk watahitaji sare ya magoli chini ya mawili au
ushindi kuweza kutinga katika hatua ya makundi
ambako kuna timu maarufu kama Manchester
United.


Kikosi cha KRC Genk
kilikuwa: Bizot, Walsh,
Dewaest, Colley, Uronen,
Heynen, Pozuelo, Ndidi,
Bailey, Buffalo/Trossard dk42
na Samatta/Karelis dk82.
Lokomotiva Zagreb: Zagorac,
Peric, Majstorovic, Rozman,
Bartolec, Sunjic, Bockaj/
Cekici dk86, Coric/Ivanusec
dk45, Fiolic, Grezda na
Maric.



Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

 
Top