Kiungo aliyeigharimu Man Utd kiasi cha Pauni milioni 89, Paul Pogba amejinasibu kuwa tayari kuanza kuitumikia klabu hiyo katika mchezo wa ligi wa mwishoni mwa juma hili ambao utawakutanisha dhidi ya Southampton.
Pogba ambaye hakuwa sehemu ya kikosi kilichofanya vyema katika mpambano wa ufunguzi wa ligi
mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Bournemouth na kupata ushindi wa mabao matatu kwa moja,
amesisitiza kuwa tayari kucheza alipohojiwa na kituo cha televisheni cha Sky Sports cha nchini England.
Kiungo huyo mwenye umri wa
miaka 23, amesema tayari
ameshafanya mazoezi ya kutosha tangu alipowasili klabuni hapo majuma mawili yaliyopita na ameona yupo fit kuwakabiliwa Southampton, ambao watafunga safari ya kuelekea Old Trafford
hapo kesho.
Hata hivyo amedai kwamba,
maamuzi ya meneja Jose Mourinho ndio yatakayotoa nafasi kwake kucheza ama kuendelea kukaa nje,
hivyo anasubiri suala hilo japo
anajihisi yupo tayari kwa
mapambano.
“Hata meneja anapaswa kuulizwa katika hili, kwangu ninajihisi nipo tayari kucheza, lakini maamuzi ya
mwisho yapo kwake hivyo
nitasubiri na kuona kama
nitapatiwa nafasi ya kuwa sehemu ya kikosi.
“Nimefanya mazoezi kwa siku 10 tangu niliporejea hapa na kwangu naona zinanitosha kucheza.” Alisema Pogba
“Nimejiandaa kikamilifu kutokana na uzoefu nilioupata wa kucheza fainali za kombe la dunia miaka miwili iliyopita, kuwa katika kikosi
cha Juventus kwa misimu mitatu, pia nimekuwa katika sehemu ya kikosi cha vijana cha Ufaransa chini
ya umri wa miaka 20 kilichoshiriki
kombe la dunia, hivyo naamini
changamoto hizi zinanipa nafasi ya kujiamini wakati wote.” Aliongeza
Pogba.
Mshabiki wengi wa soka duniani wanasubiriki kumuona Pogba akicheza tena katika kikosi cha Man
Utd, baada ya kuondoka klabuni hapo mwaka 2012 kwa kigezo cha kukosa nafasi katika utawala wa
babu Ferguson, na ujio wake kwa kipindi hiki ulikua gumzo kutokana na ada ya usajili iliyotumika kumrejesha katika himaya ya mashetani wekundu.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni