0

Arsene Wenger amesisitiza yuko tayari kutumia
Fedha kununua Wachezaji wapya kabla Dirisha la
Uhamisho halijafungwa Agosti 31.
Hadi sasa, katika kipindi hiki cha Uhamisho
kilichoanza rasmi Julai Mosi, Arsenal
imeshagomewa na Jamie Vardy wa Mabingwa wa
England Leicester City wakati Ofa yao kumnunua
Straika wa Lyon Alexandre Lacazette imegomewa
na Klabu hiyo ya France na pia nia yao
kumchukua Sentahafu wa Valencia ya Spain
Shkodran Mustafi imegota mwamba.
Matukio hayo yamewafanya Mashabiki wa Arsenal
kuamini Wenger na Klabu hawana nia kutumia
Fedha ikibidi.
Akihojiwa nini kinajiri kuhusu Mustafi, Wenger
alijibu: “Naamini ni bora tusizungumzie kuhusu
Wachezaji binafsi lakini sisi tunafanya kazi kwa
bidii. Nyie mnaamini kabisa kuwa sipo tayari
kutumia Fedha lakini nakuhakikishia tupo tayari
kutumia Fedha!”



Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

 
Top