Mkufunzi mkuu wa klabu ya Al Ahly ya Misri
amejiuzulu chini ya mwaka mmoja baada ya
kuteuliwa kuongoza klabu hiyo.
Mholanzi Martin Jol amejizulu baada ya kuhudumu
kwa miezi sita pekee akisema anahofia usalama
wake.
Mashabiki wa klabu hiyo walionekana kukerwa
sana na kushindwa kwa timu hiyo kufika hatua ya
nusufainali Ligi ya Mabingwa Afrika.
Jol alijibizana na mashabiki Ijumaa iliyopita baada
ya timu yake kutoka sare 2-2 na klabu ya Zesco
United na kuzima matumaini yao ya kusonga
mbele.
Tangu wakati huo amepokea vitisho pia kupitia
mitandao ya kijamii jambo ambalo anasema
limechangia uamuzi wake wa kuondoka.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni