0

Meneja wa klabu ya Tottenham Hotspurs ya
Uingereza Mauricio Pochettino amemelezea kiungo
wa kati wa klabu hiyo kutoka Kenya Victor
Wanyama kama "mnyama".
Amesema mchezaji huyo ana sifa, nguvu na uwezo
wa kuifaa sana klabu hiyo msimu huu.
"Ni mnyama, ninamfahamu vyema kwa sababu
nilimnunua nikiwa Southampton kutoka Celtic. Ni
rahisi sana kutambua sifa hizi," alisema.
Meneja huyo alikuwa anajibu maswali kuhusu
umuhimu wa mchezaji huyo kwa klabu hiyo
kwenye kikao na wanahabari katika kituo cha
mafunzo cha klabu hiyo London.
Pochettino, raia wa Argentina, alijiunga na Spurs
Mei 2014 kwa mkataba wa miaka mitano na Mei
mwaka huu aliongeza mkataba huo na kuahidi
kusalia White Hart Lane hadi 2021.
Wanyama alinunuliwa £11m na Spurs kutoka
Southampton mwezi Juni mwaka huu na kujiunga
na Ponchettino, meneja aliyemnunua kutoka Celtic
kwa £12.5m mwaka 2013.
Kabla ya kuhamia Celtic, Mkenya huyo alikuwa
anachezea Germinal Beerschot ya Ubelgiji.



Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

 
Top