0

Bingwa wa mbio za mita 3000 kuruka viunzi na
maji kutoka Kenya Ezekiel Kemboi
amenyang'anywa medali yake ya shaba
aliyoishinda mjini Rio de Janeiro, Brazil.
Kemboi, 34, aliyemaliza wa tatu katika mbio hizo,
alikuwa amepewa nishani ya shaba.
Lakini Ufaransa ilikataa rufaa baada ya kubainika
kwamba mwanariadha huyo wakati mmoja, baada
ya kuruka kiunzi na maji, alikanyaga nje ya mstari
wakati akishiriki mbio hizo Jumatano.
Mfaransa Mahiedine Mekhissi, aliyemaliza nafasi ya
nne, amepandishwa hadi nafasi ya tatu na kupewa
nishani ya shaba.
Kemboi, aliyeshinda Olimpiki za London 2012
katika michezo ambayo Mahiedine Mekhissi-
Benabbad alishinda fedha, tayari ametangaza
kwamba atastaafu.
Mshindi wa mbio hizo za Rio alikuwa Mkenya
Conseslus Kipruto ambaye pia aliweka rekodi
mpya ya Olimpiki , muda wake ukiwa 8:03.28.
Mmarekani Evan Jager alimaliza wa pili muda wake
ukiwa 8:04.28.
Muda wa Kemboi ulikuwa 8:08.47 na wa Mekhissi
8:11.52.



Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

 
Top