Riyad Mahrez amesaini miaka minne kuitumikia
Leicester City hadi mwaka 2020.
Ni jana tu alitaarifu kuwa anaweza kuondoka
klabuni hapo kama timu 'flani flani' zitamtaka.
Yaonekana ilikuwa anataka mkataba wake 'mnono'
uharakishwe.
Mahrez, Morgan, King na Vardy wote sasa
wamesaini mikataba mipya sambamba na kocha
wao Claudio Ranieri.
Leicester ina kazi kubwa msimu huu, licha ya
kukabiliwa na ushindani mkubwa kwenye Premia
Ligi, ina kibarua kingine kwenye michuano ya ligi
ya mabingwa Ulaya.
Timu hiyo imeanza msimu mpya wa Premia kwa
kuchapwa mabao 2-1 na timu iliyo na hali mbaya
kiuchumi, Hull City ambayo imerudi kwenye
Premia msimu huu.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni