Mabingwa wa Hispania, FC Barcelona wametwaa
taji la Super Cup baada ya kuilaza Sevilla mabao
3-0 katika mchezo uliopigwa usiku wa kuamika leo
kwenye dimba la Nou Camp.
Barca iliingia katika mchezo huo ikiwa tayari na
mabao mawili ambapo ilipata ushindi wa 2-0 katika
mchezo wa kwanza uliopigwa siku tatu zilizopita.
Arda Turan aliifungia FC Barcelona mabao mawili
huku jingine likifungwa na Lionel Messi.
Barca imetwaa taji hilo tena baada ya mara ya
mwisho kulitwaa mwaka 2013.
Baada ya mchezo huo, La Liga inaanza rasmi
kesho kwa michezo miwili ambapo Malaga
itachuana na Osasuna huku Deportivo ikiumana na
Eibar.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni