Mshambuliaji wa Liverpool, Mario Balotelli
amekutana na kocha wa wake wa zamani Inter
Milan, Jose Mourinho kuomba ushauri pia akitaka
aunganishwe na timu.
Hata hivyo hakuna uwezekano wa Liverpool
kujiunga na Manchester United, imefahamika.
Balotelli anataka kumtumia Mourinho kama 'refa
wake' ili apate timu kwa haraka.
Mtukutu huyo mwenye umri wa miaka 26 hatakiwi
na kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp na tayari
alishamwambia atafute timu.
Tangu asajiliwe na Liverpool miaka miwili iliyopita,
hajaweza kuonyesha cheche zake.
Msimu uliopita alitolewa kwa mkopo AC Milan.
Akiwa Milan alifunga mabao matatu tu kutoka
michezo 23 hata hivyo alikumbana na majeraha
yaliyomuweka nje ya dimba kwa miezi mitatu.
Balotelli alitamba na Manchester City msimu
2010/11 na 2011/12 akiwa mmoja wa wachezaji
walioiwezesha Manchester City kutwaa taji lake la
kwanza la ligi kuu ya Uingereza chini Roberto
Mancini wakati huo.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni