Nahodha wa Azam FC, John Bocco, amesema
ushindi walioupata juzi katika mchezo wa Ngao ya
Jamii dhidi ya Yanga ni ishara ya namna
walivyojipanga kusaka ubingwa wa Ligi Kuu Bara
msimu 2016/17.
Bocco alisema kuwa kocha wao amewaandaa
vizuri kwa ajili ya kupambana na hatimaye kutwaa
ubingwa wa ligi hiyo unaowaniwa na klabu 16
kutoka mikoa mbalimbali nchini.
“Ushindi huu utatupa mwanzo mzuri kwenye ligi,
tutaanza tukiwa na morali ya hali ya juu,” alisema
Bocco.
Hata hivyo, Bocco alisema timu yao haikuwa vizuri
katika kipindi cha kwanza ambao wapinzani wao
Yanga walifanikiwa kupata mabao mawili ya
kuongoza, lakini waliporejea tena uwanjani
walibadilika na kufanikiwa kusawazisha.
“Tunajitahidi kufuata maelekezo wa walimu wetu,
na hata kwenye mechi hii (juzi) tulibadilika kipindi
cha pili, baada ya kugundua tulipokosea, tutaenda
hivi hivi mpaka kwenye kwenye ligi,” Bocco
alisema.
Azam itaanza kampeni ya kuwania ubingwa wa
Bara kwa kuwakaribisha African Lyon waliorejea
kwenye ligi hiyo kwenye Uwanja wa Azam
Complex, ulioko Chamazi Dar es Salaam.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni