Liverpool imekubali dau la pauni mil 27 kutoka
Crystal Palace kwa ajili ya mshambuliaji wake
asiye na namba Christen Benteke.
Benteke anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya leo
Ijumaa kabla ya kukamilisha usajili wake huko
London.
Hata hivyo, thamani ya mchezaji huyo inaweza
kuzidi pauni mil 30, kulingana na makubaliano ya
timu hizo.
Palace imekuwa ikisaka mbadala wa Bolasie
aliyeuzwa Everton.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni