0

Mwanariadha Mjamaica Usain Bolt ameshinda mbio
za mita 200 katika michuano ya Olympics huko
Rio nchini Brazil na kujinyakulia medali ya
dhahabu ya pili baada ya kunyakua ya michuano
ya mbio za mita 100.
Ameshinda kwa kirahisi mbio hizo za mita 200
kwa kutumia sekunde 19.79. Bolt kwa sasa
anahitaji kushinda mbio za mita 4x 100 za
kupokezana vijiti ili kukamilisha medali ya tatu ya
dhahabu kama alivyofanya katika michuano
iliyopita.
Mapema wiki hii alidhihirisha kuwa ni mwamba wa
mbio fupi pale aliposhinda mbio za mita 100 na
kunyakuwa medali ya dhahabu.
Katika matokeo mengine Marekani imenyakulia
medali nyingine nne za dhahabu ikiwemo ya
mwanariadha wake Ashton Eaton.



Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

 
Top