Raundi ya kwanza ya ligi kuu ya England
inakamilishwa na mchezo wa leo wa London
Derby baina ya Chelsea wanaowakaribisha
mahasimu wao West Ham katika dimba la
Stamford Bridge.
Wachezaji wapya wa Chelsea Michy Batshuayi na
N’Golo Kante wanategemewa kuanza leo usiku.
Kurt Zouma anabaki kuwa nje ya uwanja kwa
majeruhi ya muda mrefu.
Kocha wa West Ham Slaven Bilic amesema Dimitri
Payet hatoweza kucheza mechi yote baada ya
kuchelewa kurudi kwenye pre-season.
Aaron Cresswell na Manuel Lanzini watakuwa nje
kutokana na majeruhi lakini Andre Ayew na
Sofiane Feghouli wanaweza kuanza.
TAKWIMU ZA MCHEZO
Chelsea hawajapoteza mchezo hata mmoja
wa nyumbani dhidi ya West Ham katika mechi
10 zilizopita. Wameshinda 7 na wametoa
sare 3.
Wagonga nyundo mara mwisho kushinda
Darajani ni mnamo September 2002 wakati
Paolo Di Canio alipofungq goli la ushindi wa
3-2.
CHELSEA
Chelsea walipata jumla ya point 50 msimu
uliopita – hizi ni points chache walizowahi
kupata mabingwa watetezi wa Premier
League.
Endapo watashindwa kupata ushindi leo
itakuwa wamecheza mechi 6 za nyumbani
bila ushindi kutokea msimu uliopita – itakuwa
mara ya kwanza kwa tangu walipocheza
mechi 12 kutoka November 1994 na April
1995.
The Blues wana jumla ya point 51 kutoka
kwenye mechi zao za ufunguzi za Premier
League, pointi hizi ni zaidi ya timu yoyote.
Antonio Conte hajafungwa katika mechi 28 za
ligi za nyumbani akiwa kocha wa klabu tangu
January 2013. (W26, D2).
Chelsea wameruhusu angalau goli moja katika
kila mechi ya nyumbani tangu walipowafunga
Norwich 1-0 mnamo November 2015.
West Ham United
West Ham walimaliza nafasi ya juu zaidi
kwenye ligi kwa mara ya kwanza katika
kipindi cha miaka 20.
West Ham walipata point 15 kwenye London
derbies msimu uliopita, pointi nyingi zaidi
kuliko klabu yoyote ya London. Chelsea
waliishia kupata point 12.
Wagonga Nyundo wamefunga angalau goli
moja katika mechi zao 13 zilizopita.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni