0

Mo Farah amekuwa mwanariadha wa kwanza wa Uingereza wa mbio za
uwanjani kushinda nishani 3 za dhahabu kwenye michezo ya Olimpiki! Hii ni baada ya kuwabwaga Wakenya na
Waethopia kwenye mbio za mita 10,000 zilizofanyika mjini Rio.
Mwanariadha huyo ana umri wa miaka 33 na alijikwaa wakati wa mbio hizo
japo alijikakamua vilivyo kwenye mita 100 za mwisho na kushinda kwa muda wa dakika 27.5. Paul Tanui wa Kenya
ameshinda nishani ya fedha,
mwanariadha wa Ethopia, Tamirat Tola akimaliza wa 3.


Sasa Farah atarejea uwanjani Jumatano kutetea taji lake la mbio za mita 5,000 aliloshinda miaka minne iliyopita mjini
London. “Nimeshinda dhahabu 3 kwa wanangu watatu!” Farah alisema.
“Ningetaka kushinda dhahabu ya 4 katika mbio za mita 5,000 kwa mtoto wangu mchanga!”
Iwapo atashinda mbio hiyo basi atafikia mafanikio sawa na ya mwanariadha wa Finland, Lasse Viren aliyetwaa mataji
mawili ya Olimpiki kwenye mbio za mwendo mrefu mwaka 1976. Hata hivyo Mo Farah alipata ushindani mkubwa
kutoka kwa Mkenya, Paul Tanui na ilimbidi atumie nguvu za ziada ili kutoboa.



Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

 
Top