Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Yusuph Manji
ametangaza kujiuzulu wadhifa huo kutokana na
madai kuwa amekuwa akisakamwa na watu
mbalimbali hasa baada ya kuweka bayana azma
yake ya kuikodisha Yanga kwa miaka 10.
Kwa mujibu wa taarifa iliyosambaa mapema leo
kwenye mitandao ya kijamii, Manji anasema
amechoshwa na masimango anayoyapata kutoka
kwa watu ambao wengine ni rafiki zake huku
wengine wakiwa viongozi wa Yanga licha ya ukweli
kwamba amekuwa akiifadhili klabu ya Yanga kwa
mapenzi yake, amedai hakuna faida aliyoipata.
"Natukanwa sana na baadhi ya matajiri ambao ni
wapenzi wa Yanga. . Hawapendi mimi niwepo pale.
. Pesa ni yangu natoa kwa mapenzi niliyonayo kwa
klabu yangu.
"Kwanini nitukanwe wakati sipati maslahi yoyote?
najiuzulu," amesema Manji.
Kwa mujibu wa taarifa iliyothibitishwa na mmoja
wa viongozi wa Yanga, klabu hiyo imeitisha kikao
cha dharura kitakachowahusisha viongozi wote wa
Kanda pamoja na wanachama wa klabu hiyo.
Kikao hicho kitafanyika kesho Jumanne saa nne
asubuhi na baada ya kikao hicho klabu hiyo itatoa
taarifa rasmi kuhusu sakata hilo.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni