0

Staika wa zamani wa Simba na Stand United, Elias
Maguri ambaye sasa anaitumikia timu ya Dhofar ya
nchini Oman, ameendelea kufanya vizuri akiwa na
kikosi hicho.
Juzi Jumatatu, mshambuliaji huyo aliongoza timu
hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya Oman kuibuka na
ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki dhidi
ya timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 23 ya
nchi hiyo.
Hiyo ilikuwa ni mara ya pili kwa Maguri kuiongoza
timu yake hiyo kuibuka na ushindi ambapo mara
ya kwanza alifanya hivyo katika mchezo wa kirafiki
dhidi ya AL Etihad ambayo ipo daraja la pili na
sasa inatafuta nafasi ya kupanda ligi kuu.
Maguri alisema kuwa anajivunia hali hiyo kwani
inamfanya azidi kuongeza bidii anapokuwa
uwanjani ili aweze kuwa na nafasi ya kudumu
katika kikosi cha timu hiyo itakayomwezesha
kuonwa na klabu nyingine za ndani na nje ya nchi
hiyo.
“Namshukuru sana Mungu kwani maendeleo
yangu tangu nimefika hapa siyo mabaya sana na
nimekuwa nikifunga katika mechi zote nilizocheza
ambapo leo (juzi Jumatatu), tulikuwa na mechi ya
kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya vijana chini ya
miaka 23, nimeifungia timu yangu bao moja
ambalo tulipata katika mchezo huo.
“Lakini pia kama wiki mbili zilizopita, niliifungia pia
timu yangu bao moja katika ushindi wa mabao 2-1
tulioupata, hivyo najivunia hali hiyo na
ninamuomba Mungu anijalie niendelee hivihivi,”
alisema mshambuliaji huyo.



Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

 
Top