0

Mchezaji wa Judo kutoka Misri Islam El Shehaby
amerudishwa nyumbani kutoka katika michezo ya
Olimpiki baada ya kukataa kusalimiana kwa mkono
na mpinzani wake Sasson kutoka Israel baada ya
pigano lao.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 alipewa
adhabu hiyo na kamati ya michezo ya Olimpiki
baada ya kupoteza katika raundi ya kwanza siku
ya Ijumaa.
Kamati ya Olimpiki imesema kuwa tabia yake
inaenda kinyume na sera ya urafiki iliopo katika
maadili ya michezo hiyo.
Kamati ya Olimpiki ya Misri ilimshtumu El Shehaby
na kumrudisha nyumbani.
El Shehaby baadaye alizomwa na mashabiki
waliokuwa wamejaa katika ukumbi wa mchezo huo
na alitakiwa kurudi katika ukumbi huo ili kutoa
heshima kwa mpinzani wake kwa kuwa ni kinyume
na sheria za mchezo huo.
Sasson hatahivyo alibaini kwamba makocha wake
walimuonya kwamba El Shehaby huenda
asimsalimie kwa kushikana mikono.
Inadaiwa kwamba raia huyo wa Misri alikuwa
ameshinikizwa na baadhi ya mashabiki wake
kutoka nyumbani kutoshiriki katika pigano hilo.



Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

 
Top